Home Tetesi za Usajili GHANA YATAJA KIKOSI CHA AWALI CHA WACHEZAJI 27-NAHODHA JONH MENSAH ATEMWA

GHANA YATAJA KIKOSI CHA AWALI CHA WACHEZAJI 27-NAHODHA JONH MENSAH ATEMWA

1510
0
SHARE
_74798682_schlupp
BEKI wa klabu ya Leicester City , Jeffery Schlupp ameitwa katika kikosi cha awali cha wachezai 26 cha timu ya Taifa ya Ghana `Black Stars` kwa ajili ya kombe la dunia mwezi ujao nchini Brazil.
 Schlupp ameichezea Ghana katika mechi moja tu, lakini kiwango chake cha sasa kimeisaidia Leicester kupanda ligi kuu nchini England.
 Pia mshambuliaji wa Helsingborg , David Accam ni mchezaji mwingine ambaye imeshangaza kujumuishwa katika kikosi hicho baada ya kuifungia klabu yake mabao 10 katika michuano ya ligi ya Sweden.
 Kocha wa Ghana,  Kwesi Appiah amewaacha baadhi ya wachezaji wenye majina makubwa akiwemo nahodha John Mensah  na Isaac Vorsah.
 
Michael Essien amechaguliwa kushirikia kombe la dunia kwa mara ya pili baada ya kukosa la mwaka 2010 kutokana na majeruhi, wakati huo huo Asamoah Gyan na Sulley Muntari wapo katika mazingira ya kutokea katika mashindano ya kombe la dunia kwa mara ya tatu.
 
The Black Stars wataanza mazoezi mjini Accra mei 20 mwaka huu kabla ya kusafiri kwenda Amsterdam kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya  Uholanzi mei 30.
 
Appiah amesema atapunguza wachezaji mpaka kufikia 23 kabla ya kwenda Marekani kufaya maandalizi ya mwisho huko Miami.
 Mechi ya mwisho ya kirafiki kwa Ghana itakuwa dhidi ya  korea kusini mjini Miami kabla ya kusafiri kwenda Brazil juni 11, siku tano kabla ya mechi yao ya ufunguzi ya kundi G dhidi ya Marekani.
Pia watachuana na Ujeruani na Ureno katika kundi lao.
KIKOSI CHA GHANA HIKI HAPA 
 
Walinda Mlango: Fatau Dauda (Orlando Pirates), Adam Kwarasey (Stromsgodset), Stephen Adams (Aduana Stars).
Mabeki: Samuel Inkoom (Platanias), Daniel Opare (Standard Liege), Harrison Afful (Esperance), Jeffrey Schlupp (Leicester), John Boye (Rennes), Jonathan Mensah (Evian), Jerry Akaminko (Kisehirspor), Rashid Sumalia (Mamelodi Sundowns).
Viungo: Michael Essien (AC Milan), Sulley Muntari (AC Milan), Rabiu Mohammed (Kuban Krasnodar), Kwadwo Asamoah (Juventus), Emmanuel Agyemang-Badu (Udinese), Afriyie Acquah (Parma), Christian Atsu (Vitesse), Albert Adomah (Middlesbrough), Andre Ayew (Marseille), Mubarak Wakaso (Rubin Kazan).
 
Washambuliaji: Asamoah Gyan (Al Ain), Kevin-Prince Boateng (Schalke 04), Abdul Majeed Waris (Valenciennes), Jordan Ayew (Sochaux), David Accam (Helsingborg).

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here