Home Tetesi za Usajili NIGERIA YATANGAZA KIKOSI CHA AWALI CHA WACHEZAJI 30 KOMBE LA DUNIA

NIGERIA YATANGAZA KIKOSI CHA AWALI CHA WACHEZAJI 30 KOMBE LA DUNIA

1168
0
SHARE

1399450651-b Kocha wa Nigeria, Stephen Kheshi

SHIRIKISHO la Soka Nigeria (NFF) limetangaza kikosi cha cha awali cha wachezaji 30 kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia la FIFA nchini Brazil baadaye mwaka huu.

Kutangazwa kwa wachezaji hao jana, kumefutia kikao cha pamoja baina ya NFF na kocha wa Super Eagles, Stephen Keshi.

Kikosi hicho ni makipa; Vincent Enyeama, Austin Ejide, Chigozie Agbim na Daniel Akpeyi; Mabeki: Elderson Echiejile, Juwon Oshaniwa, Godfrey Oboabona, Azubuike Egwuekwe, Kenneth Omeruo, Joseph Yobo, Kunle Odunlami na Efe Ambrose.

Viungo: John Mikel Obi, Ogenyi Onazi, Ramon Azeez, Joel Obi, Nosa Igiebor, Michael Uchebo, Ejike Uzoenyi, Sunday Mba na Reuben Gabriel, wakati washambuliaji ni: Ahmed Musa, Shola Ameobi, Emmanuel Emenike, Obinna Nsofor, Osaze Odemwingie, Babatunde Michael, Victor Moses, Uche Nwofor na Nnamdi Oduamadi.
Nigeria ni moja kati ya nchi tano za Afrika zitakazoshiriki fainali za Kombe la dunia mwaka huu, pamoja na Algeria, Ghana na Ivory Coast.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here