Home Kitaifa MAMBO YALIPUKA, RAIS MPYA SIMBA SC KUPATIKANA JUNI 29

MAMBO YALIPUKA, RAIS MPYA SIMBA SC KUPATIKANA JUNI 29

1981
0
SHARE

_DSC0696Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
MAMBO yaiva!. Kamati ya uchaguzi ya Simba imepanga uchaguzi mkuu wa klabu hiyo kufanyika juni 29 mwaka huu baada ya msajili wa vyama vya michezo na klabu kuipitisha katiba yao iliyofanyiwa marekebisho.
Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya Simba yalipopo mtaa wa Msimbazi Kariakoo, jijini Dar es salaam leo mchana, mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya Simba sc, mwanasheria na wakala wa wachezaji wa FIFA, Dkt. Damas Ndumbaro amesema kamati yake imekutana jana na kuamua tarehe hiyo ya uchaguzi ili kupata rais mpya, makamu wa rais na wajumbe wapya wa kamati ya utendaji.
“Kamati yangu ina watu makini na wenye uadilifu mkubwa. Pia wana mawazo ya kuijenga klabu ya Simba”.
“Jana tulikutana na kupanga ratiba ya uchaguzi. Hatutakuwa na huruma na watu watakaoenda kinyume na kanuni za uchaguzi”. Alisema Ndumbaro.
Ndumbaro alisema kuanzia mei 9 mwaka huu mchakato wa kuanza kutoa fomu kwa watu wenye nia ya kuwania nafasi za uongozi utaanza rasmi, na siku ya kurudisha fomu ni mei 14 mwaka huu.
Mei 17 mwaka huu kamati ya uchaguzi itafanya zoezi la kuhakiki fomu za wagombea wa nafasi mbalimbali ndani ya klabu ya Simba.
Aidha, Ndumbaro aliongeza kuwa mei 19 mwaka huu kamati yake itatangaza majina ya wagombea na mei 20 watafungua milango ya pingamizi dhidi ya wagombea.

rage 2Ismail Aden Rage safari yake yaelekea ukingoni Simba

Mei 25 mwaka huu kamati ya uchaguzi itaanza kusikiliza pingamizi na mei 27 zoezi la usaili wa wagombe litaanza.
Mei 29 kamati ya uchaguzi ya Simba itatangaza matokoe ya usaili na mei 30 masuala ya maadili yataangaliwa.
Baada ya zoezi hilo, Ndumbaro alisema juni 2-9 mwaka huu zoezi likalofanyika ni kukata rufaa kamati ya rufaa na juni 10-12 rufaa zitasikilizwa.
Juni 16, 2014 zoezi litakuwa ni kukata rufaa kamati ya rufaa ya maadili, na juni 16-20 maamuzi ya mwisho ya kamati ya rufaa na kamati ya rufaa ya maadili yatafanywa.
Baada ya hapo juni 21 orodha ya mwisho ya wagombe itatangazwa na juni 24-28 kampeni za kunadi sera kwa wagombe zitaanza.
Juni 29 ni siku ya uchaguzi ambapo Simba itapata rais mpya atayerithi mikoba ya mpiganaji Ismail Aden Rage.
Hii itakuwa siku muhimu sana kwa wana Simba wote na wanachama ndio wenye mamlaka ya kuamua nani aiongoze klabu hiyo baada ya sinema nyingi kuonekana katika uongozi wa Rage.
Rage amekuwa akilaumiwa kwa muda mrefu na baadhi ya wanachama wa Simba kwa madai kuwa ameshindwa kukidhi matarajio yao, lakini sasa safari yake iko ukiongoni.
Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya viongozi na timu kufanya vizuri uwanjani, bila shaka wanachama mtachagu viongozi wazuri.
Safar njema kwa Simba kuelekea katika uchaguzi wenu. Amani itawale kwa muda wote.

Soma www.bkmtata.blogspot.com

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here