Home Kitaifa WAFANYAYO AZAM FC SAFARI HII, WAKONGWE SIMBA, YANGA MPO?

WAFANYAYO AZAM FC SAFARI HII, WAKONGWE SIMBA, YANGA MPO?

914
0
SHARE

azam bingwaNa Baraka Mpenja, Dar es salaam

Tel: 0712461976
MABINGWA wa soka Tanzania bara, Azam fc wamezidi kuonesha weledi mkubwa katika uendeshaji wa klabu yao.
Ni ngumu kuwaelewa Azam jinsi wanavyofanya maamuzi juu ya mambo yao ya msingi kuhusu klabu na wachezaji wao.
Kwasababu watanzania wengi wanasumbuliwa na unazi wa Simba na Yanga, ni ngumu sana kuelewa kirahisi unapotaka kuzungumza suala kama hili.
Tangu imeingia katika soka la ushindani msimu wa 2008/2009, wachezaji wengi wa Kitanzania na kigeni wamepita Azam.
Lakini somo kubwa la kujifunza ni namna wanavyoondoka katika klabu hii.
Tunashuhudia katika soka la ulaya, timu zikiwa na mawasiliano ya mapema na wachezaji wanaotaka kuwaondoa klabuni.
Inatakumika busara kubwa kuzunguza na wachezaji wasiowahitaji na kuwapa taarifa za mapema ili wahangaikie maisha mengine kama wanaona bado wana uwezo wa kucheza.
Ashley Cole wa Chelsea anamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu, na siku ya jumapili katika mchezo wa klabu yake na Nowrich alipewa heshima kubwa baada ya mechi.
Sababu ya mashabiki na viongozi wa Chelsea kumpatia heshima hiyo ni utumishi uliotukuka katika klabu hiyo kwa kipindi cha miaka mingi.
Lakini kitu cha msingi, Cole alishaambiwa mapema kuwa hataongezewa mkataba, na ndio maana alimwaga machozi jumapili wakati akiwaaga mashabiki.

article-2620086-1D92D35A00000578-419_634x431Mfano wa Cole hautoshi, ipo mingi ambayo watu wote wanaopenda mpira wanajua na hakuna haja ya kuitaja kwa leo.
Lakini Ulaya nako kuna matatizo yake juu ya kuwaacha wachezaji hasa wa rangi nyeusi.

Wazungu kwa hili hawawezi kukwepa lawama. Kuna wakati wanafanya maamuzi mabaya sana kwa wachezaji wa Kiafrika.
Wengi wanaamini kuwa ni ubaguzi wa rangi, yawezekana ndiyo.
Kumbuka suala la Didier Drogba akiwa Chelsea, Yaya Toure na Samuel Eto`o wakiwa Barcelona.
Wachezaji hawa wa Kiafrika walizifanyia kazi kubwa mno klabu zao na kuelekea kuvunja rekodi za wazungu, lakini jinsi walivyoachwa kwa dharau pengine wangekuwa weupe mambo yasingekuwa hivyo.
Samir Nasir, kiungo wa Manchester na timu ya taifa ya ufaransa, kuna wakati aliwahi kukariririwa na vyombo vya habari kuwa kama Yoya Toure angekuwa mzungu basi angekuwa akitajwa kuwa kiungo bora zaidi wa ukabaji duniani.
Nasri alimaanisha rangi ya yaya Toure inamfanya asipewe heshima hiyo na watu wa rangi nyeupe.
Tuachane na hayo, yapo mengi ya kusema juu ya namna ya kuacha wachezaji katika klabu.
Lakini ulaya kwa asilimia nyingi wana weledi, japokuwa kuna changamoto kama nilivyosema hapo juu.
Tukirudi nyumbani Tanzania, jana uongozi wa klabu ya Azam FC umefikia makubaliano ya kuvunja Mkataba na mshambuliaji wake kutoka Ivory Coast, Ismail Kone ambaye alikuwa anamaliza Novemba mwaka huu.
Moja ya vitu vya msingi kuvieleza katika maamuzi hayo ni kama yafuatayo;
Mosi; namna Azam walivyozungumza na mchezaji wao kwa kumweleza ukweli na hatimaye kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba.
Kone ni raia wa Ivory Coast ambaye alisajiliwa kwa malengo makubwa na Azam, lakini imekuwa tofauti na matarajio ya klabu.

koneKlabu imeona haihitaji huduma yake, si kwa maana ya kushuka kiwango, hapana!, bali ni kutofiti katika mfumo wa klabu kwa sasa.
Ilielezwa kuwa Pande zote mbili zimefikia makubaliano na mchezaji huyo amepewa haki zake na kurejea nchini mwao.
Angalia jambo hili, Kone anaitwa na uongozi wa Azam fc na kuelezwa wazi kuwa klabu haina mpango naye, wanajadili kwa pamoja na kukubaliana kauvunja mkataba kwa njia ya amani.
Kizuri zaidi haki zake zote anapewa na kuaga. Sidhani kama Kone akienda kwao ataizungumza vibaya Azam fc kwasababu wamemheshimu kwa kiwango cha juu.
Zimezoeleka sinema kwa klabu za Simba na Yanga. Unajua ni wachezaji wangapi wanazidai klabu hizi?
Unajua kwanini TFF walikuwa wanakata mapato ya Yanga mechi za mwishoni mwa msimu?
Unakumbaka sakata la akina John Njoroge, Wisdom Ndlovu, Steven Malashi, juzi juzi akina Mwasyika, Nsajigwa na wengineo.
Ipo mifano mingi sana. Hata Simba nao ni hatari sana, wapo wachezaji wengi wanaodai chao na hawajalipwa mpaka leo.
Nadhani kutolipwa haki zao kunatokana na weledi mdogo wa wachezaji wa kitanzania kujua namna ya kudai chao.
Lakini kwa wale wanaotokea nje ya nchi wamekuwa wakiwahenyesha sana viongozi wa Simba na Yanga.
Kwa miaka mingi, Simba na Yanga wanavunja vibaya mikataba na wachezaji wao na kutowatendea haki hata kidogo.
Hii inatokana na kukosekana kwa weledi kwasababu kuvunja mkataba na mtu sio vita.
Watoto wao Azam fc wanaelekea sehemu nzuri sasa. Watu watanuna kwa hili, lakini ukweli uko hivyo. Usinune kwasababu tu unapenda Yanga na Simba, hivyo ukiona hoja kama hii inahisi kuna unazi kwa mwandishi.
Cha msingi inapotokea mambo ya weledi mkubwa namna hii kwa Azam fc, lazima tuikubali changamoto hii.
Pili; Azam FC imewashukuru kwa mchango wao wachezaji wake wanne, Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo, Malika Ndeule na Omar Mtaki kwa kipindi chao chote walichoitumikia klabu hiyo.
Wanne hao wamemaliza mikataba yao na hawataongezewa- klabu inawashukuru kwa mchango wao kwa kipindi chote tangu wajiunge nayo.
Azam FC pia imepokea na kuyakubali maombi ya wachezaji wake wawili, Samih Haji Nuhu na Luckson Kakolaki kustaafu kwa sababu mbalimbali.
Nuhu anasumbuliwa na maumivu ya goti ambalo hana matumaini ya kupona karibuni, wakati Kakolaki ameamua kustaafu ili achukue mafunzo ya ukocha.
Klabu imempa ajira ya kudumu Nuhu katika moja ya viwanda vyake, wakati Kakolaki ameingizwa kwenye benchi la Ufundi la akademi ya klabu.
Kama umesoma vizuri aya za hapo juu, utakuwa umejifunza kitu kikubwa mno kutoka kwa Azam fc.
Cha kwanza ni kujua kutoa shukurani kwa wachezaji waliofanya kazi katika klabu, lakini utumishi wao umefika kikomo na klabu haina mpango wa kuendelea nao.
Hakuna kitu kizuri kama mtu kuheshimu mchango wako. Hata katika maisha ya kawaida, unapopewa asante kwa jambo ulilofanya, huwa inatia moyo.
Kuachana na mchezaji sio ugomvi, lazima umheshimu na kuongea naye kwa busara.
Japokuwa hawaongezewi mikataba, lakini nadhani hawana chuki kabisa kwasababu kwanza wamejua mapema na usajili bado kuanza, hivyo wanao uwezo wa kutafuta kazi sehemu nyingine.
Mara ngapi wachezaji wanaachwa dakika za mwisho za usajili katika klabu kongwe za Simba na Yanga”
Unategemea watajipanga muda gani” madhara yake wanaweza kukosa msimu unaofuata.
Pia angalia Azam walivyomfanyia kitu kikubwa beki wake Samih Haji Nuhu.
Majeruhi ya goti yamemfanya astaafu soka. Azam wamemhangaikia sana mpaka kwenda naye Afrika kusini kumfanyia upasuaji.
Lengo lilikuwa ni kumrudisha uwanjani mapema, lakini jitihada zimegonga mwamba.
Baada ya hapo Uongozi ukaona umpe ajira ya kudumu kwenye moja ya kiwanda cha Azam. Hivi unaelewa kitu gani hapa?, ni kujua namna ya kutoa fadhila.
Wachezaji wangapi wa Simba na Yanga wamepotea baada ya kupata majeruhi?.
Kiggi Makasi, Victor Costa, Stephano Mwasyika…………………….ni wengi sana na mnawajua. Wako wapi na waliachajwe na klabu zao na jitihada gani zilifanyika kuwatibu.
Unaweza kusema mbona wengine walipelekwa India, nenda kazungumze nao wakueleze ukweli.
Nimefanya mahojiano na wengi wao jinsi klabu zilivyowafanyia huko India, ni aibu kubwa sana na ukitaka nitakupa ushahidi huo.
Lakini kwa Nuhu maisha mengine yataendelea kwasababu ya kuheshimiwa na kupewa ajira baada ya viongozi kujua haweza kurudi uwanjani mapema.
Siku ya mechi ya Taifa stars dhidi ya Burundi, Azam walimleta Nuhu uwanja wa Taifa akiwa katika baiskeli yake ili aitazame mechi hiyo.

MALINZI NA SAMIHHili lilikuwa jambo zuri sana, hivi Kiggi Makasi aliletwa na Simba? Nini hatima yake katika klabu hiyo? Najua hayupo kwenye mipango ya kocha, lakini nini klabu yake imemfanyia? Hatufahamu.
Unakumbuka alichofanyiwa Ibrahim Shikanda baada ya kustaafu soka Azam fc?, na sasa Kakolaki.
Wamebakishwa kuwa moja ya sehemu ya benchi la ufundi?. Si unaoa Giggs Man United?, hata Azam mambo haya yapo kwasasa.
Kwa wakongwe wetu wachezaji wangapi walifanya mambo makubwa na wakaachwa vibaya baada ya kumaliza kazi.
Wachache walirudi kufanya kazi baada ya kujisomesha wenyewe.
Utataja Mkwasa, Minziro, Kibadeni, na wengine, lakini uliza katika kusoma kwao walisaidiwa na klabu?
Wengi walijifanyiwa mambo yao na baadaye klabu zikaona wanaweza kuzisaidia timu na ndio maana wakaingizwa benchi la ufundi, lakini kutimuliwa imekuwa ni sehemu yao.
Sina tatizo kutimua makocha kwasababu ni utaratibu wa dunia nzima.
Kwa haya myafanyayo Azam fc, kuna funzo kubwa kwa Simba na Yanga.
Lengo la kutaja Simba na Yanga ni kwasababu ndizo klabu kubwa zaidi nchini.
Kila la heri Azam fc katika harakati zenu za kutuletea vitu vipya katika soka letu.

soma www.bkmtata.blogspot.com

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here