Home Kimataifa DECO: BARCELONA KUSHUKA KIWANGO KAWAIDA TU

DECO: BARCELONA KUSHUKA KIWANGO KAWAIDA TU

708
0
SHARE

398451_heroaNYOTA wa zamani wa Barcelona, Deco, amesema kushuka kwa kiwango cha klabu hiyo kama klabu bora ya kihistoria duniani ilitarajiwa.
Vijana wa Gerardo Martino hawako katika kiwango kama misimu ya nyuma na msimu huu walitolewa hatua ya robo fainali ya UEFA.
Pia walikosa kombe la mfalme ( copa de Rey) na sasa hawana matumaini ya kutwaa ubingwa wa La Liga na kuwaachia kinyang`anyiro mahasimu wawili, Real Madrid na Atletico Madrid.
Deco aliyecheza Camp Nou kati ya mwaka 2004 na 2008 anadhani Barcelona hawajachanganyikiwa na matokeo mabaya msimu huu, kwani wamekuwa wakionesha juhudi kubwa hasa katika michezo mikubwa.
“Ni ngumu kujua yanayoendelea Barca ukiwa nje. Watu wanasema mengi, lakini kwa upande wangu kinachotokea ni kawaida katika michakato ya mpira”. Deco ameliambia gazeti la Marca.
“Barca wamepata makombe mengi miaka ya karibuni, wamekuwa katika kiwango cha juu-walikuwa ni klabu bora zaidi duniani kwa mujibu wa watu wengi”.
“Kwa kinachowatokeo sasa ni kawaida na wanapata uzoefu mzuri kuwa kwenye soka kuna wakati mgumu pia”.
“Klabu inatakiwa kujipanga upya kusaka mafanikio zaidi, iwabakishe nyota kama Lioel Mess na Andres Iniesta ambao ni wachezaji muhimu kwa klabu”.
“Hakuna haja ya kubadili mfumo wa uchezaji kwasababu ya matokeo mabaya”.
“ Tayari Barca wamekuwa na mpira wao na wanaweza kuuendeleza kama ilivyotokea kipindi cha Louis van Gaal, Frank Rijkaard na Pep Guardiola walivyofanya”.
“Mfumo wao ni kumiliki mpira na kwa hilo wao ndio bora zaidi duniani”. Alisema Deco.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno alikiri hakushangaa kuona Barcelona wanatolewa hatua ya robo fainali msimu huu, lakini alishangazwa kuona Atletico Madrid wakiwatoa Wakalunya.
“Ilinishitua kwa Barca kundolewa UEFA. Kwa upande wangu niliwapa kura ya kutwaa ubingwa”. Deco alisema.
“Lakini sikushangazwa na waliowatoa Barca: Atletico. Wamekuwa na kitu cha ziada msimu huu, huo ndio ukweli”.
Baada ya kuwafunga Barca hatua ya robo fainali, Atletioc waliwatoa Chelsea jumatano ya wiki hii na watakutana fainali na Real Madrid mei 24 mwaka huu mjini Lisbon, Ureno.

Soma www.bkmtata.blogspot.com

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here