Home Kimataifa WALCOTT: KUSHINDA FA KUTATUPA `MZUKA` ZAIDI WA MAKOMBE

WALCOTT: KUSHINDA FA KUTATUPA `MZUKA` ZAIDI WA MAKOMBE

883
0
SHARE

355368_heroaWINGA hatari wa Asernal, Theo Walcott anaamini kushinda taji la FA itakuwa kichocheo cha kushinda mataji mengi misimu ijayo.

Imepita miaka 9 sasa tangu Arsene Wenger abebe `ndoo` ambapo kwa mara ya mwisho aliifunga Manchester United kwa penati na kutwaa kombe la FA mwaka 2005.

Asernal wanayo fursa ya kufuta ukame huu watakapokutana na Hull City katika mechi ya fainali ya FA mei 17 mwaka huu na Walcott anaamini wakishinda italeta upepo mpya Emirates.

“Kama tutashinda FA kwa kuzingatia jinsi tunavyocheza sasa, wachezaji watakuwa na hamu ya makombe zaidi. Walcott ameiambia Tovuti ya Asernal.

“Nadhani kombe la kwanza ni muhimu- ukishinda, utashinda mengi zaidi. Nina uhakika na hilo”.

“Itakuwa heshima kwa bosi wetu kushinda kombe tena”.

“Ametuami kwa miaka yote. Kama hatuchezi vizuri, siku zote ananyoshewa vidole hata kama ni makosa yetu”.

Asernal walianza kwa kasi msimu huu na kutabiriwa kushinda taji la ligi kuu nchini England, lakini waliyeyuka mithiri ya barafu na kuziachia Chelsea, Man City na Liverpool ziendelee kupambana.

Walcott hajapangwa tangu mwezi januari mwaka huu kutokana na majeruhi, lakini anaamini kurejea kwa Aaron Ramsey, Jack Wilshere na Mesut Ozil kutaweza kutimiza ndoto zao kuelekea fainali ya FA.

Aliongeza: “Kuwakosa Aaron, Mesut, na Jack, kocha wetu alisema itakuwa ngumu kuzoeana. Ukiwatoa wachezaji hao watatu kwenye kikosi, timu itaathirika”.

“Ilikuwa huzuni kwa kila mtu kuwapoteza wachezaji hawa kwa wakati mmoja, lakini lazima mjitahidi kukaza”.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here