Home Kitaifa STEVEN MAZANDA: BADO NINA DENI NA MBEYA CITY FC, AFYA YANGU INAIMARIKA

STEVEN MAZANDA: BADO NINA DENI NA MBEYA CITY FC, AFYA YANGU INAIMARIKA

1299
0
SHARE

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
KIUNGO matata wa Mbeya City fc, Steven Mazanda ataendelea kuitumikia klabu yake hiyo msimu ujao wa ligi kuu soka Tanzania bara kutokana na kubakiwa na mwaka mmoja katika mkataba wake.
Mazanda ameuambia mtandao huu kuwa bado anadaiwa na klabu yake na kwa bahati mbaya malengo yake hayakutimia msimu uliopita baada ya kuishia nafasi ya tatu katika msimamo.
“Kitu kikubwa ni maslahi. Lakini sidhani kama Mbeya City watashindwa kunipa kile ninachohitaji”.
“Nimesikitishwa sana na timu yangu kushika nafasi ya tatu. Tulikuwa na malengo ya ubingwa, lakini haijatokea”.
“Mechi zote za mwisho sikucheza kwasababu ya majeruhi ya mguu wangu wa kulia, nadhani nitakuwepo msimu ujao kuendeleza harakati”. Alibainisha Mazanda.
Hata hivyo, Mazanda aliongeza kuwa kwasasa anaendelea kujitibu mguu wake wakati huu wa likizo.
“Ninaendelea na matibabu ya mguu wangu. Hali sio mbaya kwasasa kwasababu napiga mazoezi mepesi mepesi ili kujiimarisha afya yangu”. Alisema Mazanda.
Mazanda ambaye ni chaguo la kwanza katika nafasi ya kiungo namba nane kwa kocha Juma Mwambusi hakusita kuwashauri vijana wa Mbeya City fc kuwa maslahi ni kitu cha kwanza katika mpira, lakini waangalie sana aina ya timu zinazowahitaji.
“Unaweza kutoka Mbeya City ukaenda klabu nyingine kwa kufuata maslahi, lakini ukakosa nafasi ya kucheza”
“ Ni vizuri kufikiria vizuri unapoamua kuondoka ili usije kumaliza soka lako”.
“Siogopi kucheza timu nyingine kwasababu ukijituma unapata namba. Cha msingi tujipange vizuri”. Alisema Mazanda.

soma www.bkmtata.blogspot.com

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here