Home Kitaifa OFFICIAL: FRANK DOMAYO ASAINI AZAM FC MIAKA MIWILI

OFFICIAL: FRANK DOMAYO ASAINI AZAM FC MIAKA MIWILI

1580
0
SHARE

Katika kipindi cha masaa 24 mabingwa wa Tanzania bara klabu ya Azam FC imeipa mapigo mawili takatifu wapinzani wao Dar Young Africans baada ya kufanikiwa kumsajili mshambuliaji Didier Kavumbagu jana na leo hii Azam wamekamilisha rasmi usajili wa kiungo Frank Domayo.

Taarifa rasmi zilizotolewa na klabu ya Azam ni kwamba Domayo amesaini mkataba wa miaka miwili wa kujiunga na mabingwa wa VPL baada ya kumaliza mkataba wake wa miaka mwili na Yanga.

Domayo anakuwa mchezaji wa pili kuondoka rasmi Yanga ndani ya siku mbili – huku kukiwa na taarifa kwamba mchezaji mwingine anayetajwa kuondoka jangwani ni aidha Emmanuel Okwi au Mbuyu Twite.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here