Home Kimataifa KAULI YA GUARDIOLA BAADA YA KIPIGO KUTOKA KWA REAL MADRID

KAULI YA GUARDIOLA BAADA YA KIPIGO KUTOKA KWA REAL MADRID

1214
12
SHARE

PEP Guardiola ameeleza kuwa kiwango walichoonesha Bayern Munich ni kikubwa mno japokuwa walifungwa mabao 4-0 na Real Madrid katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya UEFA kwenye uwanja wa Allianz Arena jana.
The Bavarians walichanganyikiwa kwa mabao mawili ya Sergo Ramosi na Cristiano Ronaldo na kuvuliwa ubingwa kwa wastani wa mabao 5-0 kufuatia kupigwa bao 1-0 mchezo wa kwanza Santiago Bernabeu.
Guardiola ambaye kikosi chake kilicheza kwa kujituma zaidi katika kipigo cha kwanza cha bao 1-0 Bernabeu, hakikuweza kufua dafu jana Allianz Arena.
“Kila kitu kinatokea katika mpira kutokana na kucheza vizuri. Nimefungwa mara nyingi katika kazi yangu na hii ni mojawapo”. Guardiola amewaambia waandishi wa habari.
“Tulifungwa mabao mengi, lakini tulicheza kwa kiwango kikubwa na ndio sababu ya kupoteza”.
“Hakuna sababu nyingine, huu ndio mpira”.
“Unapocheza vibaya, unafungwa mabao mengi. Tuliingia na nguvu, tungeweza kufunga kwa nafasi tulizopata, lakini hatukuweza”.
“ Kucheza kwetu vibaya ndio sababu pekee ya kufungwa”.
Bayern imefanikiwa kutwaa kombe la dunia la klabu na Bundesliga msimu huu, na wamebakiwa na kombe la mwisho la DFB-Pokal mei 17 dhidi ya Borussia Dortmund.
Hii itakuwa kama marudio ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya mwaka jana.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here