Home Kitaifa KAGERA SUGAR KUTAFUTA MSAIDIZI WA THEM FELIX NJE YA NCHI

KAGERA SUGAR KUTAFUTA MSAIDIZI WA THEM FELIX NJE YA NCHI

1056
0
SHARE

DSC04328 (1)Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
WAKATA miwa wa Kaitaba, `Wanankulukumbi` Kagera Sugar wanatarajia kufanya usajili makini ili kuendana na kasi ya ushindani katika mitanange ya ligi kuu soka Tanzania bara msimu ujao.
Murage Kabange, kocha msaidizi wa Kagera Sugar amebainisha mapungufu kadhaa katika kikosi chao na sasa wapo katika mipango ya kufanyia marekebisho.
“Kwanza majeruhi ya kudumu kwa baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza ni tatizo lilituathiri sana”.
“Pili ubutu wa safu ya ushambuliaji lilikuwa tatizo la kudumu kwa Kagera Sugar mpaka tunapozungumza hivi”.
“Tatu hatukuwa na wachezaji mbadala, kwahiyo kila inapotokea mchezaji muhimu anapata majeruhi, ilikuwa janga kwetu”.
Kutokana na matatizo hayo, Kabange alisema wanatarajia kuongeza nguvu sehemu ya ushambuliaji ambapo wanafikiria kutafuta hata mchezaji wa kigeni.
“Tunadhani ipo haya ya kwenda hata nje ya nchi ili kupata washambuliaji watakaotuongezea nguvu msimu ujao”.
“Lakini tunafirikia kutafuta wachezaji wengi ili tuwe na machaguo mengi zaidi. Tutasajili vijana zaidi ili iwe rahisi kufundishika”. Alisema Kabange.
Kagera Sugar waliomaliza msimu uliopita katika nafasi ya tano kwa pointi 38 walikuwa wanamtegemea mshambuliaji wao nyota, Them Felix `Mnyama` ambaye hata hivyo hakuonesha makali sana.
Pia Kabange alieleza kuwa wanafikiria kuboresha safu yao ya ulinzi na kiungo.
Kagera Sugar walifungwa mabao 20 katika mechi 26, huku wakifunga mabao 23.
Kwasababu hiyo, Kabange alisema kuna haja ya kupunguza mabao ya kufungwa msimu ujao kwa kutafuta wachezaji watakaoongeza nguvu katika ngome yao ya ulinzi.
Hata hivyo, Kabange alisema mabao 23 ya kufunga katika mechi 26 yanadhihirisha ubutu wa safu ya ushambuliaji na kwa kushirikiana na kocha mkuu, Mganda Jackson Mayanja wameona kuna haja ya kutafuta washambuliaji wakali.
Aidha, aliongeza kuwa msimu ujao wanatarajia kuingia katika mbio za ubingwa au nafasi tatu za juu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here