Home Kitaifa OFFICIAL: DIDIER KAVUMBAGU ASAINI AZAM FC MWAKA MMOJA

OFFICIAL: DIDIER KAVUMBAGU ASAINI AZAM FC MWAKA MMOJA

1328
0
SHARE

Mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi aliyekuwa anakipiga kwenye klabu ya Dar Young African Didier Kavumbagu amesaini kuichezea klabu bingwa ya Tanzania bara Azam FC.

Taarifa rasmi zilizothibitishwa na mtandao huu kupitia meneja wa klabu ya Azam FC Jemedari Said ni kwamba Kavumbagu ambaye inaaminika amemaliza mkataba wake wa miaka miwili na klabu ya Yanga aliosaini wakati akitokea kwao Burundi miaka miwili iliyopita, amesaini mkataba wa mwaka mmoja tu kuitumikia klabu ya Azam FC.

“Kavumbagu is a done deal! Tumemalizana nae na amesaini rasmi mkataba wa mwaka mmoja, so tutakuwa nae msimu ujao kwenye kampeni ya kutetea ubingwa wetu pamoja na michuano ya klabu bingwa ya Afrika,” alifunguka Jemedari

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here