Home Kitaifa MATOGOLO WA MBEYA CITY AFUNGUA MILANGO KWA AZAM, SIMBA, YANGA….

MATOGOLO WA MBEYA CITY AFUNGUA MILANGO KWA AZAM, SIMBA, YANGA….

1091
0
SHARE

Antony Matogolo mwenye jezi namba 16 mgongoni wakati wa mechi yao na Azam fc uwanja wa sokoine jijini Mbeya

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
KIUNGO wa ulinzi wa Mbeya City fc, Antony Matogolo amebainisha kuwa kama timu yoyote itamhitaji na kumhakikishia maslahi mazuri anaweza kuondoka katika klabu yake hiyo iliyotikisa soka la Bongo msimu uliopita.
Akizungumza na mtandao huu, Matogolo amesema mpira ni maisha yake na inapotokea sehemu yenye maslahi mazuri zaidi hana budi kwenda.
“Kwa upande wangu mimi, soka ni maisha, halafu ni kazi. Hata wewe kwenye kazi yako inapotokea mtu mwingine mwenye maslahi mazuri anakuhitaji, haina budi kwenda sehemu unayoona itakusaidia zaidi”.
“Ni kweli naipenda timu yangu, naiamini, nawaamini viongozi wake na walimu wanaonifundisha, bado nina mkataba na Mbeya City fc”.
“Siwezi kusema nitaondoka kwa sasa hivi, lakini ikitokea, ninaweza kuangalia sehemu nyingine yenye maslahi mazuri”. Alisema Matogolo.
Matogolo amebainisha kuwa inapotokea mchezaji anatoka klabu moja kwenda nyingine anakutana na changamoto kwasababu anakutana na watu wengine na makocha tofauti, lakini kwa upande wake kikubwa ni kupambana.
“kuhama sio lazima, kwasababu unatakiwa kuangalia, je, huko ninakoenda nitapa nafasi na kuendelea kutumika”.
“ Kwahiyo unapotaka kuhama lazima uangalie vitu vingi zaidi ya maslahi”. Alisema Matogolo.
Kiungo huyo aliyepanda hewani aliongeza kuwa yeye anaweza kucheza timu yoyote ile.
“Kwa mfano wanavyocheza Azam fc hawawezi kucheza kama Mbeya City kwasababu ina wachezaji tofauti na makocha tofauti wenye falsafa tofauti”.
“Lakini ukijipa muda wa kujifunza unaweza kuendana na mfumo mpya”. Alisema Matogolo.
Aidha, mtaalum huyo wa kutibua mipango ya wapinzani kueleka eneo lao la hatari alisema kwasasa anaendelea na mazoezi ya kawaida kuendelea kujiweka fiti.
“Mazoezi ninayofanya kwasasa ni tofauti na ninapokuwa na klabu yangu. Kwasasa naweza kufanya mara moja kwa siku na kuendelea na shughuli nyingine”.
“Nakutana na watu wengine ninaokaa nao mtaani, lakini mazoezi si makali sana” Alisema Matogolo.
Akizungumzia nafasi ya tatu waliyoshika msimu huu, Matogolo alisema walistahili kwasababu ya uchanga wao japokuwa malengo yao hayakutimia.
“Ulikuwa msimu wetu wa kwanza, changamoto zilikuwa nyingi. Lakini tutakuja tena na mashabiki waendelee kutuamini”. Alihitimisha Matogolo.

Soma www.bkmtata.blogspot.com

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here