Home Kimataifa GWIJI LA SOKA UJERUMANI: SIDHANI KAMA FALSAFA YA GUARDIOLA ITAWAPA BAYERN UBINGWA...

GWIJI LA SOKA UJERUMANI: SIDHANI KAMA FALSAFA YA GUARDIOLA ITAWAPA BAYERN UBINGWA UEFA

763
0
SHARE

NYOTA wa zamani wa soka la Ujerumani, Stefan Effenberg ameonesha wasiwasi wake kama falsafa ya Pep Guardiola itaisaidia Bayern Munich kutwaa ubingwa wa UEFA wakati huu ambapo mchezaji muhimu Frank Ribery yupo katika kiwango cha chini.
The Barvarians walipoteza nusu fainali ya kwanza kwa bao 1-0 dhidi ya Real Madrid wiki iliyopita uwanja wa Santiago Bernabeu na wameshuka kiwango tangu walipotawazwa mabingwa wa Bundesliga mwezi machi mwaka huu.
Effenberg anaamini falsafa ya sasa ya Bayern ya kupiga pasi nyingi haikuweza kuwasaidia Bernabeu na ana wasiwasi katika mechi ya leo ambapo wachezaji muhimu wanashindwa kuonesha makali yao kama msimu uliopita.
‘Bayern wameshinda asilimia 90 ya mechi zao”.
“Katika mechi za Bundesliga, walizitesa timu pinzani kwa kumiliki zaidi mpira. Kwa kiwango kikubwa ni mfumo tofauti wa Bayern”.
“Timu kama Manchester United, Real Madridi au Chelsea zinaweza kujilinda vizuri na kupata matokeo”. Gwiji huyo wa Ujerumani ameuambia mtandao wa Goal.com
“Bayern wamekuwa kwenye ubora mkubwa, hivyo kubeba mataji matatu ni hadhi yao. Lakini walishindwa kuwa na kasi dhidi ya Real Madrid”.
“Kila muda Bayern wanahitaji mpira na kupiga pasi mbele ya boksi kama mpira wa mikono.”
“Mchezo huu umepoteza mwelekeo, wangine wanasema `unaboa`, wengine wanasema ni wa vilevile na hakuna mabadiliko”.
“Frank Ribery hana makali kama mwaka jana. Mpira wao umedumaa kwasababu ya kushuka kiwango kwa nyota huyu”.
Effenberg amewaonya Bayern kuwa watulivu katika mchezo wa leo.
“Sidhani kama wameshapoteza. Wachezaji wana ubora wa juu. Watakapo kuwa 0-0 watatakiwa kuwa watulivu na kupangilia mashambulizi yao”.
“Wanaweza kufunga bao dakika ya 85. Wachezaji wasije wakachanganyikwa na kujisahau. Wachezaji watajua nini cha kufanya”.
Borrusia Dortmund waliifunga Real Madrid mabao 2-0 katika mechi ya marudiano ya robo fainali baada ya kufungwa mabao 3-0 uwanja wa Bernabeu, lakini Effenberg amewaonya Bayern kutoiga takwimu hizo.
“Nadhani Madrid watatumia zaidi mfumo wao wa kushambulia kama kawaida. Lakini Carlo Ancelotti ameshaweka wazi kuwa wataacha Bayern wacheze mpira na kutumia makosa yao”.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here