Home Kimataifa CECH, TERRY, ETO`O, HAZARD WAIPASHIA ATLETICO MADRID KESHO

CECH, TERRY, ETO`O, HAZARD WAIPASHIA ATLETICO MADRID KESHO

1189
0
SHARE

Inashangaza: Petr Cech akitembea na Nathan Ake (katikati) na Marco van Ginkel kuelekea katika mazoezi.

JOSE Mourinho ameanza maandaliza ya mechi ya kesho ya nusu fainali ya pili ya UEFA dhidi ya Atletico Madrid, huku ikishangaza kumuona mlinda mlango namba moja wa Chelsea, Petr Cech akifanya mazoezi.

Cech aliteguka beka katika mchezo wa kwanza uliomalizika kwa suluhu ya bila kufungana Vicente Calderon na Mourinho alithibitisha wiki iliyopita kuwa kipa huyo anahitaji upasuaji ili kurudisha bega katika hali yake.

article-2615784-1D71868C00000578-845_634x454Nyota wa samba: Willian, David Luiz, Ramires na Oscar wakielekea katika uwanja wa Coham tayari kwa mazoezi.

Haikuwa rahisi kumouna Cech leo hii ambaye alitakiwa kukaa nje ya uwanja kwa miezi mitatu, hivyo imeshangaza kumuona mchezaji huyo akiwa miongoni mwa wachezaji waliofanya mazoezi leo hii.

Alipoulizwa kama yuko imara kwa mechi ya kesho, alitabasamu na kusema “Ndiyo”, lakini alienda zake na kujiunga na wenzake.

Cech alionekana akifanya mazoezi mepesi leo hii, na makipa wenzake Mark Schwarzer, Henrique Hilario na Mitchell Beeney walipoanza mazoezi na kocha wa makipa, Christophe Lollichon, Cech alikaa pembeni.
Mbali na Cech, wachezaji wengine waliokuwa majeruhi, Samuel Eto`o, nahodha, John Terry, na Eden Hazard nao wamefanya mazoezi leo hii kujiandaa na kipute cha kesho.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here