Home Kimataifa MNUSO WA NAFASI YA NNE WANUKIA KWA ASERNAL, YAILAZA NEWCASTLE 3-0

MNUSO WA NAFASI YA NNE WANUKIA KWA ASERNAL, YAILAZA NEWCASTLE 3-0

633
0
SHARE

ASERNAL imezidi kujiweka katika mazingira mazuri ya kuingia timu nne bora za ligi kuu soka nchini England msimu huu na kufuzu kucheza UEFA mwakani baada ya usiku huu kuilaza Newcastle mabao 3-0 kwenye uwanja wa Emirates.
Mabao ya Laurent Koscielny, Mesut Ozil na Olivier Giroud yameifanya Asernal iweke pengo la pointi nne dhidi ya wapinzani wao wakubwa wa nafasi ya nne, klabu ya Everton.
Kwa matokeo hayo, Asernal imefikisha pointi 73 katika nafasi ya nne, huku Everton wakisalia nafasi ya tano kwa pointi 69, na timu zote zimebakisha mechi mbili mbili kufunga msimu.

article-2615255-1D6DFEB000000578-209_634x378Asernal hawakutarajia kama wangekuwa hapo walipo kufuatia kuanza vizuri ligi kuu msimu huu na walionekana kuchanganyikiwa zaidi baada ya kufungwa katika uwanja wa Goodison Park.
Wiki tatu baadaye, Everton walianza kuteteleka na Asernal kurudi katika moto wake baada ya kurejea kwa nyota wake Aaron Ramsey na Mesut Ozil.
Kumaliza katika nafasi ya nne jumlisha kombe la FA yatakuwa mafanikio kwa kocha Aserne Wenger msimu huu na pengine yatachangia kumwaga wino katika mkataba mpya wa kuifundisha klabu hiyo.
Asernal wanaweza kujihakikishia nafasi ya nne kama wataifunga West Bromwich Albion jumapili ya wiki hii, huku wakisubiri mechi yao ya kufunga msimu dhidi ya Norwich.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here