Home Kitaifa MINZIRO ATOA MBINU ZA MAFANIKIO KWA WANANDINGA, MAKOCHA BONGO

MINZIRO ATOA MBINU ZA MAFANIKIO KWA WANANDINGA, MAKOCHA BONGO

989
0
SHARE

Kocha mkuu wa JKT Ruvu, Fredy Felix Minziro (wa kwanza kushoto)  Taifa

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
KOCHA wa JKT Ruvu ya mkoani Pwani, Fredy Felix Minziro amebainisha kuwa makocha wanakumbana na hali ngumu katika ufundishaji wa soka nchini kwasababu wachezaji wengi hawajatokea katika `akademi` za mpira.
Katika mahojiano maalum na mtandao huu, Minziro amesema wachezaji wengi walikosa mafunzo ya soka utotoni, hivyo kujikuta wakiwa katika hali ngumu ya kuelewa misingi ya mpira wakati huu wa utu uzima.
“Pamoja na hayo, walimu hatupaswi kuchoka. Lazima tufanye kazi ya ziada kuwasisitiza mara kwa mara mpaka watuelewe”.
“Tukisema tukate tamaa, hakuna wachezaji wa tofauti na hawa tulionao labda siku za usoni kama akademi zitajengwa kuanzia chini mpaka kitaifa”.
“Kwenye mafunzo ya ukocha, wanasema rudia hata mara 200, hata wazungu wanaelewa hivyo. Walimu lazima tukubali kuvumilia haya”. Aliongeza Minziro.
Aidha, Minziro aliwaasa wachezaji kuwa na nidhamu ya kuzingatia mafunzo na kama hawajaelewa wawe wepesi wa kuuliza.
Alifafanua kuwa kuna baadhi ya wachezaji wanahangaika kuuliza kwa walimu na kutaka kujifunza vitu vipya na wakifundishwa wanaelelwa, lakini kuna wachezaji huwa hawana malengo hata kidogo.
Minziro alieleza kuwa mpira kwasasa umekuwa ajira nzuri inayoweza kumpatia mtu fedha nyingi, hivyo lazima wachezaji wa Kitanzania wabadilike.
“Vijana kama wanataka kucheza mpira wajikite katika mazoezi na kujiepusha na vitendo visivyokuwa na faida”.
“Wazingatie mafunzo ya walimu wao na wakubali kuvumilia kwasababu mpira ni safari ndefu”.
“Wachukulie klabu za Tanzania kama sehemu ya kupita. Wawe na malengo ya kufika mbali, na ili wafanikiwe ndoto hizo, lazima wakubali kukaa chini na kuzingatia mafunzo ya makocha wao”. Alisisitiza Minziro.

Soma www.bkmtata.blogspot.com

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here