Home Kitaifa KOCHA YANGA: HAKUNA MAPENZI YA SOKA TANZANIA, VIJANA WAWE MAKINI KUWAKOSHA MASHABIKI

KOCHA YANGA: HAKUNA MAPENZI YA SOKA TANZANIA, VIJANA WAWE MAKINI KUWAKOSHA MASHABIKI

873
0
SHARE

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
KOCHA msaidizi wa Yanga Sc, Charles Boniface Mkwasa `Master` amewashauri mashabiki wa soka nchini kuzipenda timu zao kwa wakati wote na kuepuka tabia ya kuwabebesha lawama wachezaji, mabenchi ya ufundi na viongozi yanapotokea makosa.
Mkwasa ameuambia mtandao huu kuwa tatizo la wapenzi wengi wa soka Tanzania hawana uvumilivu hususani timu inapofanya vibaya tofauti matarajio yao.
“kwa mfano unakuta timu imefungwa, wachezaji wanaenda kwa mashabiki wao ili wawasalimia, halafu ukashangaa wanarushiwa chupa za maji tofauti na wenzetu Ulaya”.
“Najua hatuwezi kufananisha kwetu na ulaya, lakini kuna makosa ya kawaida yanatokea uwanjani mfano kukosa penati”.
“Hivi ni vitu vya kawaida tu, lakini ikitokea hivyo wachezaji wanapata lawama nyingi”. Alisema Mkwasa.
Mkwasa aliongeza kuwa mazingira kama haya yanamfanya mchezaji ashindwe kujiamini anapocheza mpira.
“Baadhi ya wachezaji wakizomewa wanashindwa kujiamini kabisa, sasa hii inamfanya ashindwe kufanikisha malengo yake”.
“Tatioz ni watu kutokuwa na mapenzi ya kimpira kama wenzetu Ulaya”.
“Kwa nchi nyingi za kiafrika tatizo la mashabiki kukosa mapenzi ya dhati na timu zao lipo kwa kiasi kikubwa”.
“Wachezaji wanashangiliwa wanapofanya vizuri tu, lakini wakifanya makosa ni dhambi kubwa”. Alisema Mkwasa.
Kocha huyo aliwashauri vijana kuzidisha umakini katika kazi yao ili kuendana na mazingira ya kitanzania kwasababu kubadilika kunahitaji muda.
Mkwasa alifafanua kuwa kama vijana wanataka kushangiliwa, basi wafanye vizuri na kujituma zaidi uwanjani.
“Tatizo kubwa la wachezaji ni kukosa msingi ya mwanzo ya mpira na malengo.”.
“Unakuta mchezaji fulani ni mzuri lakini ameibukia wapi huelewi”.
“Nadhani ipo haja ya kuwaelemisha vijana kama hawa. Kama hawana misingi ya mpira toka utotoni, lazima wakubali kushaurika na kuzingatia mafunzo ya walimu wao”.
“Wakiwa watulivu katika mafunzo ya makocha wao wataepuka kuzomewa na mashabiki wao”. Alisema Mkwasa.
Aidha kocha huyo aliwataka wachezaji kutumia muda wao katika mazoezi wakati huu wa likizo ndefu kwasababu mpira uchawi wake ni bidii ya mazoezi.
“Najua wapo likizo kwasasa. Hatuwezi kuwazuia kufanya starehe kwasababu walijinyima walipokuwa kazini”
“Cha msingi kwao ni kutambua kuwa starehe ni adui mkubwa wa mpira. Lazima mchezaji ajipe muda wa mazoezi ili kulinda kiwango chake”.
“Wajitambue na wawe makini wakati huu ili wakirudi uwanjani wasianze upya na kuwapa shida makocha wao”. Alishauri Mkwasa.

Soma www.bkmtata.blogspot.com

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here