Home Kimataifa ADAM NDITI: MOURINHO ANATUFUNDISHA KULINDA, KUCHEZA , KUSHAMBULIA, TUTAWAFUNGA ATLETICO

ADAM NDITI: MOURINHO ANATUFUNDISHA KULINDA, KUCHEZA , KUSHAMBULIA, TUTAWAFUNGA ATLETICO

1320
0
SHARE

UNAPOZUNGUMZIA wachezaji wa Kitanzania wenye bahati ya kucheza klabu kubwa duniani, huwezi kuacha kumzungumzia Adam Nditi anayekipiga katika klabu ya Chelsea.
Nditi amepata bahati ya kunolewa na kocha bora duniani, Jose Mourinho katika dimba la Stamford Bridge.
Mahojiano maalum yamefanywa baina ya mtandao huu na Nditi akiwa jijini London nchini Uingereza.
Nditi amefafanua kuwa katika mazoezi wanayofanya chini ya kocha Mourinho wanafundishwa mambao matatu.
“Katika mazoezi yetu, tunafundishwa namna ya kulinda, kucheza na kufunga”
“Kocha anatumia muda mwingi katika masuala haya matatu”.
“Kila klabu ina mbinu zake za kusaka ushindi katika mechi”. Amesema Nditi.
Aidha, kinda huyo alishangazwa na maneno ya watu kuwa walicheza kwa kujilinda zaidi “maarufu kama kupaki basi `dhidi ya Liverpool jumapili iliyopita na kushinda mabao 2-0 kwenye uwanja wa Anfield.
“Watu wanasema tulipaki basi, sasa ilikuwaje tukafunga mabao mawili?, au Liverpool walijifunga?, kila timu ina mbinu zake za kutafuta matokeo”.
“Timu yetu ilijilinda ili isifungwe, ikacheza mpira na kushambulia na kupata mabao mawili”.
“Nilisema toka awali kuwa kocha Mourinho anatufundisha kulinda , kucheza mpira na kushambulia ili tufunge”.
“Tulifanya vyote, tulilinda lango letu, tukacheza mpira na kufunga”
“Hii ni mbinu ya Chelsea na kocha wetu, Jose Mourinho”.
Akiuzungumzia mchezo wa kesho kutwa dhidi ya Atletico Madrid katika nusu fainali ya pili ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, Nditi alisema wanajiamni kuibuka na ushindi.
“Mechi na Atletico timu itabadilika kiuchezaji, Usitegemee kuona mpira uliochezwa Hispania, hapa nyumbani tutacheza tofauti na kupata ushindi”. Amesema Nditi.
Chelsea katika mchezo wa kwanza ulilazimisha suluhu pacha ya bila kufungana na Atletico katika dimba la Vicente Calderon na ili kufuzu hatua ya fainali wanatakiwa kushinda bao 1-0.
Hii itakuwa mechi muhimu kwa Jose Mourinho mwenye chagizo la kushinda mchezo mgumu wa ligi dhidi ya Liverpool jumapili iliyopita.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here