Home Kimataifa NAPOLI, SABELLA `WAPANIKI` KUUMIA KWA HIGUAIN

NAPOLI, SABELLA `WAPANIKI` KUUMIA KWA HIGUAIN

908
0
SHARE

KLABU ya Napoli imekumbwa na wasiwasi mkubwa baada ya kuumia kwa Gonzalo Higuain katika mechi yao na Inter Milan hapo jana uwanja wa San Siro iliyomalizika kwa suluhu (0-0).

Mshambuliaji huyo raia wa Argentina alilazimika kutoka katika mchezo huo wa Seria A baada ya kugongana na beki wa Inter, marco Andreolli.

Napoli wamethibitisha leo hii kuwa mshambuliaji huyo wa zamani wa Real Madrid amepata majeruhi ya kifundo cha mguu na kuwa hatarini kukosa mechi ya Coppa Italia wiki ijayo.

“Amepata majeruhi makubwa sana kwenye mguu wake” amesema taarifa ya klabu.

“Majibu hayo yametokana na uchunguzi uliofanywa na madaktari wa klabu juu ya hali ya Gonzalo Higuain baada ya kugongana na Andreolli kwenye mechi ya Inter dhidi ya Napoli”.

“Higuain hayuko katika hali nzuri na tathmini zaidi ya afya yake itatolewa siku zijazo”.

Kocha wa timu ya taifa ya Argentina, Alejandro Sabella amesitushwa na majeruhi ya Higuain na anaomba apone haraka kwasababu ni moja ya washambuliaji atakaowatumia kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 26 mpaka sasa amefunga mabao 24 katika mechi 44 alizocheza tangu ajiunge na Napoli mwezi wa nane mwaka jana kwa uhamisho wa paundi milioni 40 kutoka Real Madrid.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here