Home Kitaifa KUNUSURIKA KUPOROMOKA DARAJA KWAWAPA SOMO PRISONS

KUNUSURIKA KUPOROMOKA DARAJA KWAWAPA SOMO PRISONS

681
0
SHARE

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

MAAFANDE wa Tanzania Prisons `Wajelajela` wanasubiri kwa hamu kubwa ripoti ya kocha wao, David Mwamwaja ili waanze kuandaa mikakati mapema kuelekea msimu wa 2014/2015 wa ligi kuu soka Tanzania bara.
Katika mahojiano maalum na Mtandao huu, Katibu mkuu wa Prisons, Inspekta Sadick Jumbe amesema misimu miwili mfufulizo wamenusurika kushuka daraja, hivyo malengo yao ni kusajili wachezaji wazuri ili msimu ujao washeka nafasi tano za juu.
“Sisi ni viongozi na tuna majukumu yetu. Tumeona makosa yetu, lakini inapofika mambo ya ufundi, Mwamwaja ndiye mwenye majukumu”.
“Tuna imani na kocha huyo mwenye historia kubwa katika soka. Anaandika ripoti yake ambayo tutaipata ndani ya wiki moja ijayo”.
“Kwa kufuata mapendekezo yake, sisi viongozi tutatekeleza kila alichokiona na kumshauri kwa yetu machache tuliyoyaona kwa nafasi ya viongozi”. Alisema Jumbe.
Pia Jumbe alisema timu za majeshi zimeonakana kuwa dhaifu mno msimu huu na moja ya sababu ni kukosa maandalizi mazuri na masuala ya kiuchumi.
“Angalia kule chini wamemaliza Rhino, Oljoro pale juu yao amekuja Ashanti timu ya kiraia, halafu Mgambo na unatukuta sisi Prisons”.
“Kinachotuathiri sisi ni maandalizi duni na uhaba wa fedha”.
“Pia aina ya wachezaji tulionao. Sisi tunachukua raia, wakifika wanajituma sana, lakini wakiwa maaskari wanaona sasa mpira sio kazi tena”
“Kinachozibeba timu za kiraia ni wachezaji kutambua kuwa mpira ni kazi yao na wakifanya vibaya watakosa kwa kwenda. Lakini kwetu ni tofauti kabisa”.
“Vijana wamekuwa wazembe sana hususani wanapopata kazi kwasababu wanajua wakishuka daraja, wataendelea kupata mshahara kwa kazi yao ya uaskari”. Alisema Jumbe.
Jumbe aliongeza kuwa timu za majeshi zinaonekana kutokuwa na mvuto kwa mashabiki wengi wa soka kwasababu ya aina ya kazi yao.
“Sisi maaskari ya magereza, kazi yetu ni kutunza wahalifu. Angalia Polisi kazi yao ni kushika wahalifu. Hali hii imezitenganisha timu na waanchi”.
“Kwa mfano mtu akisikia Mbeya City fc anaona ni timu yake, lakini akisia Tanzania Prisons anaona kama timu ya Tanzania nzima. Hapana! Prisons ipo Mbeya na kila kitu kinafanyika Mbeya”
“Ili kuhakikisha tunairudisha timu kwa wananchi, Prisons tumefungua matawi maeneo tofauti.
“Tuna matakiwa Uyole, Mwanjelwa, Mabatini, Sinde, Isanga na maeneo mengi.”
“Matawi yapo maeneo mengi, angalia mechi yetu ya mwisho na Ashanti United. Mashabiki walisafiri kutoka matawini na kuja Morogoro. Tunawakaribisha watu waje kujiunga na Prisons”. Alisema Jumbe.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here