Home Kimataifa GIGGS AANZA MAMBO MAN UNITED, AILAZA NOWRICH 4-0, ROONEY, MATA WAMPA UKOCHA...

GIGGS AANZA MAMBO MAN UNITED, AILAZA NOWRICH 4-0, ROONEY, MATA WAMPA UKOCHA WA KUDUMU

1526
0
SHARE

RYAN Giggs ameanza vizuri kazi yake akiwa meneja wa muda wa Manchester United baada ya kuilaza Nowrich City mabao 4-0 katika mechi ya ligi kuu soka nchini England kwenye uwanja wa Old Trafford.
Wayne Mark Rooney amefunga mabao mawili, huku Juan Mata aliyeanzia benchi leo hii naye akifunga mabao mawili.
Giggs ambaye kwa muda mrefu ameitumikia klabu ya Man United akiwa mchezaji, aliteuliwa kuwa kocha mkuu wa muda baada ya David Moyes kufukuzwa kazi jumanne ya wiki hii.
Matokea ya leo ni mabaya mno kwa Nowrich City kwasababu yanawaweka katika hatari ya kushuka daraja, huku wakibakiwa na mechi ngumu dhidi ya Asernal na Chelsea.

article-2613799-1D61DF3000000578-499_634x383Baada ya mechi ya leo, Nowrich wanabakia katika nafasi ya 17 kwa pointi zao 32 kufuatia kushuka dimbani mara 36.
Man United wanabakia nafasi yao ya 7 kwa kujikusanyia pointi 60 baada ya kucheza mechi 35.
Rooney baada ya kuchangia ushindi wa leo amesema kuwa anaamini Giggs ana kila sifa ya kuwa meneja wa kudumu wa Manchester United.
“Ilikuwa tofauti kabisa leo chini ya Giggs”. Rooney ameuambia mtandao wa Sky Sports.
“Nimecheza naye kwa miaka 10, lakini wote tunajua kuwa ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa na amekuwa sehemu ya benchi la ufundi msimu uliopita”.
“Anajijenga kuwa kocha. Sisi kama timu tunaona hilo”
“ Tunaona jinsi alivyoanza majukumu yake baada ya kuteuliwa”
“ Imekuwa furaha kupata ushindi mbele yake”. Amesema Rooney muda mfupi baada ya mechi kumalizika.
Rooney ameongeza kuwa kila kitu kipo chini ya bodi kwasababu wao ndio wenye mamlaka ya kuchagua nani kuwa kocha mkuu na hakuna anayejua, lakini Giggs anastahili kushika nafasi hiyo.

article-2613799-1D616FC300000578-110_634x585Mata kwa upande wake baada ya kutokea benchi na kufunga mabao mawili amesema ana furaha ya kufanya kazi chini ya Giggs.
“Kwa upande wangu ninajisikia furaha kufanya kazi chini yake”.
“Tangu nikiwa mdogo, nakumbuka alikuwa anacheza.”
“ Ni mtu mzuri wa Man United. Unaweza kusema alizaliwa hapa na nadhani wachezaji wote wanajisikia vizuri kuwa naye katika mazoezi”.
“Lakini lipo juu ya uwezo wetu, maamuzi ni juu ya bodi. Acha tufurahi tukiwa naye mpaka mwisho wa msimu”. Alisema Mata.

MATOKEO YA MECHI ZOTE HAYA HAPA CHINI

ENGLAND: Premier League  
14:45 Finished Southampton 2 – 0 Everton      
17:00 Finished Fulham 2 – 2 Hull City      
17:00 Finished  Stoke City 0 – 1 Tottenham      
17:00 Finished Swansea 4 – 1 Aston Villa      
17:00 Finished West Brom 1 – 0 West Ham      
19:30 Finished Manchester United 4 – 0 Norwich

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here