Home Kimataifa KOCHA BARCELONA TITO VILANOVA AFARIKI DUNIA

KOCHA BARCELONA TITO VILANOVA AFARIKI DUNIA

967
0
SHARE

TANZIA!. Wakati klabu ya FC Barcelona ikiwa na matatizo ya uwanjani wiki za karibuni, leo hii machungu yameongezea zaidi baada ya kocha wake wa zamani, Tito Vilanova kufariki dunia kwa ugonjwa wa saratani akiwa na miaka 45.

Kwa muda mrefu Tito alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa saratani na alilazimika kujiuzulu kufundisha soka na kuendelea na matibabu mpaka leo hii alipotangulia mbele ya haki.

Ameondoka mapema sana, ghafla na akiwa kijana mno. Tito atabaki kuwa alama na shujaa Camp Nou.

Tito alipelekwa chumba cha dharula jana kwa upasuaji baada ya hali yake kugeuka na kuwa mbaya wiki iliyopita.
Vilanova amekuwa akisumbuliwa na saratani tangu Novemba mwaka 2011 na Radio Nacional imesema alikuwa katika wakati mgumu siku mbili hizi
Klabu ya FC Barcelona imeandika katika akaunti yake ya twita: “FC Barcelona ipo katika huzuni. Tito Vilanova amefariki akiwa na umri wa miaka 45. Apumzike kwa amani,”.
Kocha huyo alilazimika kujiuzulu mwaka 2013 baada ya kuanza kuzidiwa na maradhi hayo.
Timu yake ilishinda taji la La Liga, lakini Jordi Roura aliifundisha Barcelona kwa miezi miwili wakati Vilanova aliposafiri kwenda New York kwa matibabu ya saratani, kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na Tata Martino msimu huu.
Vilanova aliteuliwa kuwa kocha wa Barcelona mwishoni mwa msimu wa 2011-12 na akawawezesha Blaugrana kusawazisha rekodi ya Real Madrid kumaliza msimu na pointi 100. Alianza kuwa Msaidizi wa Pep Guardiola mwaka 2008.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here