Home Kitaifa COASTAL UNION MOTO WAZIDI KUWAKA, AFISA HABARI ABWAGA MANYANGA

COASTAL UNION MOTO WAZIDI KUWAKA, AFISA HABARI ABWAGA MANYANGA

821
0
SHARE

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
AFISA habari wa klabu ya Coastal Union, Hafidh Kido ametangaza kubwaga manyanga kutokana na migogoro inayoendelea katika klabu hiyo.
Akiongea na mtandao huu jioni ya leo, kido amesema kitaaluma yeye ni mwandishi wa habari na hatakiwa kuwa upande wowote, hivyo ameamua kujitoa katika nafasi yake.
“Kila nilichokuwa nakifanya Coastal ilikuwa ni kujitolea na si kwa masilahi. Coastal ni klabu yangu na sikuwa na mkataba, lakini nimefanya kazi zao bila tatizo kwasababu naipenda timu hii”. Alisema Kido.
Kido aliongeza kuwa maamuzi yake ameyachukua bila kushinikizwa na mtu yoyote.
Haya yamekuja siku chache baada ya aliyekuwa mfadhili wa klabu hiyo, mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Bin Slum Tyres, Nassor Bin Slum Bin Slum kuondolewa na uongozi wa klabu hiyo.
Bins Slum leo hii amesema ataendelea kuwepo Coastal Union kwa kutoa msaada pale itakapobidi.
“Kama viongozi makini watakuwepo nitajitahidi kuisaidia timu yangu kwasababu mimi ni mwanachama, lakini kwa uongozi wa sasa siwezi kutoa kitu chochote”.
“Mimi sikuwa mdhamini, nilikuwa mfadhili kwa maandeleao ya klabu. Viongozi wamesema maneno mabaya juu yangu, lakini ni changamoto tu. Nitahakikisha nipo Coastal Union”.
Bin Slum amesema kwamba ametumia zaidi ya Sh. Milioni 300 kwa ajili ya Coastal Union ya Tanga ndani ya kipindi cha miaka minne, lakini ajabu malipo yake kukashifiwa.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here