Home Kitaifa AZAM YAIBANA CECAFA KUSHIRIKI MICHUANO MIPYA

AZAM YAIBANA CECAFA KUSHIRIKI MICHUANO MIPYA

877
0
SHARE

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
BARAZA la vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limeanzisha mashindano mapya ya klabu ambayo yatakuwa yanashirikisha mabingwa wa kombe la FA au washindi wa pili wa ligi kuu.
Taarifa ya CECAFA inafafanua kuwa mashindano hayo yanaanza mwaka huu na kwa mara ya kwanza yatafanyika nchini Sudan kuanzia mei 20 hadi juni 15.
Gharama za mashindano hayo kuanzia tiketi, malazi, usafiri wa ndani na zawadi za washindi vitagharamiwa na CECAFA wenyewe kushirikiana na chama cha soka nchini Sudan.
Lakini Mshindano ya Kombe la Kagame yatafanyika katika ardhi ya Rwanda na nchi hiyo imeshaanza kuandaa michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya klabu ukanda huu wa CECAFA.
Kuelekea katika mashindano hayo mapya, mabingwa wapya wa ligi kuu soka Tanzania bara, Azam fc wamepata mwaliko wa kushiriki.
Taarifa ya Azam fc kupitia Tovuti ya klabu inaeleza kuwa wataweza kushiriki michuano mipya ya klabu inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) iwapo tu itasogezwa mbele.

Katibu Mkuu wa Azam FC, Nassor Idrissa Mohammed ‘Father’ amekariri akisema kwamba wamepata mwaliko wa CECAFA kuombwa kushiriki michuano hiyo ya Mei mwaka huu, lakini wametoa jibu kwa muda uliopangwa, hawataweza.

“Tumewasiliana na CECAFA baada ya kutuomba tutume orodha ya watakaokwenda Sudan, na tumewaambia wazi kwamba muda ambao michuano imepangwa kufanyika, hatutaweza, ila kama watasogeza mbele, tunaweza kujipanga na kwenda,”alisema Father.

Father alisema kwa sasa wachezaji wa Azam FC wapo likizo hadi Juni 15 baada ya kumaliza msimu vizuri na ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, wakati michuano hiyo mipya itakayoshirikisha mabingwa wa Kombe la FA au washindi wa pili wa Ligi Kuu itafanyika nchini Sudan kuanzia Mei 20 hadi Juni 5.

Azam imemaliza Ligi Kuu na pointi 62 dhidi ya 56 za waliokuwa mabingwa watetezi, Yanga SC na kuwa timu ya kwanza nje ya Simba na Yanga kutwaa ubingwa wa Bara tangu mwaka 2000 Mtibwa Sugar ilipofanya hivyo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here