Home Uncategorized SIR ALEX KUSHIRIKI KUSAKA MRITHI WA MOYES MAN UNITED

SIR ALEX KUSHIRIKI KUSAKA MRITHI WA MOYES MAN UNITED

1105
0
SHARE

sir-alex-ferguson-spent-850-million-buying-players-at-manchester-unitedSIR ALEX FERGUSON atashiriki kikamilifu katika mchakato wa kumpata Meneja mpya wa Manchester United kuziba nafasi ya David Moyes aliefukuzwa.
Moyes, ambae alipendekezwa na Sir Alex Ferguson ili kumrithi baada ya yeye kustaafu, alifukuzwa kazi Jumanne baada ya kudumu Miezi 10 tu.
Safari hii, Ferguson atakuwa mmoja wa Watu kadhaa, hasa Wakurugenzi wa Bodi ya Man United, watakaoshiriki mchakato mzima wa kumpata Meneja mpya badala ya yeye pekee kupendekeza Jina kama alivyofanya alipoteuliwa Moyes.
Hivi sasa Man United inaongozwa na Meneja wa Muda, Ryan Giggs, ambae ni Kocha-Mchezaji wa Klabu hiyo na anasaidiwa na Wachezaji wenzake wa zamani Nicky Butt, aliekuwa akifundisha Timu ya Rizevu na Phil Neville, aliekuwa Msaidizi chini ya Moyes lakini hii Leo imetajwa kwamba Paul Scholes nae amejumuika kwenye Jopo hilo la Benchi la Ufundi.
Pia, Man United imesema inaendelea kuchambua yupi atafaa kuwa Meneja wao wa kudumu huku Vyombo vya Habari huko England vikigusia kuwa wenye nafasi kubwa ni Kocha wa Netherlands, Louis van Gaal na Meneja wa sasa wa Real Madrid, Carlo Ancelotti.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here