Home Kimataifa MOYES AWASHUKURU MASHABIKI MAN UNITED

MOYES AWASHUKURU MASHABIKI MAN UNITED

975
0
SHARE

394031_heroaDAVID Moyes amewashukuru mashabiki wa Manchester United baada ya kufukuzwa kazi jana na kusema anajivunia kuiongozo klabu kubwa duniani kama Man United.

Moyes alifukuzwa kazi kufuatia kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Everton na kuisababisha klabu hiyo ishindwe rasmi kufuzu michuano ya UEFA mwakani na kumaliza ligi ikiwa katika nafasi ya chini zaidi tangu ilipofanya hivyo msimu wa 1989-90.

Kupitia kwa chama cha makocha wa ligi kuu nchini England, Moyes amesema: “Kuteuliwa kuwa kocha wa Manchester United, moja ya klabu kubwa duniani, bado itabaki kuwa kitu maalumu kwangu na nitajivunia daima”.

“Kubeba mikoba ya klabu iliyokuwa katika mafanikio makubwa kwa muda mrefu nilijua itakuwa changamoto kubwa kwangu, lakini kamwe sikuogopa kuchukua kibarua hicho”.

“Kazi ya ukocha United ni ngumu, lakini daima mimi na wasaidizi wangu tulifanya  kazi kwa bidii. Nawashukuru kwa kutumia muda mwingi katika kazi na kuwa waaminifu kwa klabu”

“Tulikuwa na malengo na tulijitoa kuijenga klabu, japokuwa katika kipindi hiki  cha mpito, matokeo ya timu yalikuwa ni mabaya kwa mashabiki wa Man United tofauti na walivyotarajia”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here