Home Kitaifa MASHALI AWAKOMALIA MABONDI KUFANYA MAZOEZI

MASHALI AWAKOMALIA MABONDI KUFANYA MAZOEZI

1273
0
SHARE

SAM_2373Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
BONDIA bingwa wa UBO Afrika, Thomas Mashali maarufu kwa jina la `Simba asiyefugika` amewaasa wanamasumbwi wenzake kufanya mazoezi muda wote ili kujiimarisha kwa mapambano.
Mashali ameueleza mtandao huu kuwa hakuna uchawi wa kufanikiwa katika mchezo wa ngumi zaidi ya kujikita katika mazoezi ya kijiweka sawa muda wote.
“Mabondia tuna tabia ya kujisahau hasa pale tunapopata mafanikio. Wenzetu wa nchini hawana masihara kabisa”.
“Wanatambua kuwa ngumi ni ajira yao kama ilivyo kwa kazi yoyote, muda mwingi wanatumia katika mazoezi”.
“Lakini sisi tunaleta mchezo na ndio maana tukikutana nao tunashindwa kutamba”. Alisema Mashali.
Simba asiyefugika alisema kwa upande wake anajitahidi kufanya mazoezi katika `jimu` ya `Lazima ukae Gym` inayomilikiwa na mdau wa ngumi, Mawzo Njenje.
“”Namshukuru sana Mawazo na Gym yake ya `Lazima Ukae`. Nimekuwa nikikutana na wenzangu kama akina Francis Miyeyusho kuhakikisha tunajiweka sawasawa. Nafahamu kuwa mazoezi ndio uchawi wangu”. Aliongeza Mashali.
Aidha, Mashali aliwataka watu wote wanaopenda Masumbwi kuwa wazalendo na waungwana katika utaoaji wa zawadi katika mapambano.
“Mimi nashangaa sana niliopokuwa napigana na Japhet Kaseba mwezi uliopita kuwania ubingwa wa UBO Afrika. Kuna jamaa aliahidi Gari kama Kaseba atashinda, lakini nikishinda mie anaondoka na gari yake”.
“Huu si uanamichezo. Gari ingeahidiwa kwa yeyote atakayeshinda. Kumuahidi mmoja ni ubaguzi na inaonesha kutokomaa katika michezo. Narudia watu kama hawa si mwanamichezo”. Alisisitiza Mashali.
Pia aliitaka serikali kupitia wizara yenye dhamana kusimamia michezo kuhakikisha inawasaidia mabondi wake hasa katika mapambano ya kimataifa.
“Kuna wakati nilikuwa Afrika kusini, nikapigiwa simu kuwa Mashali njoo Tanzania kuna pambano nchini Urusi. Nilipofika Tanzania nikaambiwa na rais wangu wa PST Emmanuel Mlundwa kuwa ninaenda Urusi kucheza pambano lisilo na ubingwa, raundi 8”
“Nikamwabia dola ngapi? Akaniambia nikakubali. Nikapatiwa mikataba na kusaini. Nafika Urusi nakumbana na hali tofauti”
“Naambiwa nacheza pambano la ubingwa, tena wa dunia raundi 12. Nimuuliza Mlundwa vipi? Anasema na yeye haelewi. Nilipoteza mchezo”
“Niliumia sana kwasababu ningeambiwa mapema ningejiandaa vizuri. Kuna usanii mwingi unafanyika tunapoenda nje, serikali itusaidie mabondia” Alisema Mashali.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here